Daraja la pili lalipuliwa nchini Nigeria

Haki miliki ya picha
Image caption Raia nchini Nigeria waandamana wakitaka wasichana waliotekwanyara kuwachiliwa huru.

Wakaazi wa kazkazini mashariki mwa Nigeria wanasema kuwa washukiwa wa kundi la Boko haramu wamelilipua daraja moja karibu na eneo ambalo wasichana 200 walitekwa nyara yapata mwezi mmoja uliopita.

Daraja hilo lililopo katika barabara muhimu ni la pili kuharibiwa katika kipindi cha siku mbili.

Mwandishi wa BBC nchini Nigeria amesema kuwa ulipuaji wa daraja hilo ni mpango wa wanamgambo hao kuwazuia wale wanaotaka kuwanusuru wasichana hao kutofika eneo hilo.

Mkewe rais wa Marekani Michelle Obama ameelezea utekaji nyara wa wasichana hao kama kitendo cha kihuni kinacholenga kudidimiza ndoto za wasichana hao.