Je timu ya mwisho duniani ni ipi ?

Image caption Nicky Salapu ,kipa aliyeshiriki mechi waliofungwa 31-0 na Australia

Mwaka wa 2001 timu ya Australia iliandikisha rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi katika kandanda ya kimataifa .

Australia ilifunga Samoa mabao 31 kwa nunge .

Mshambulizi wa Australia Archie Thompson,vilevile aliiingia katika daftari za kumbukumbu kama mfungaji mabao mengi zaidi katika mechi ya kimataifa alipofunga mabao 13.

Mvua hiyo ya mabao iliipelekea American Samoa kushuka ngazi na kujikita katika nafasi ya mwisho ya orodha ya mataifa yanayocheza kandanda ya kimataifa kwa zaidi ya miaka 10.

Serikali,ya taifa hilo ilichukua jukumu la kumtafuta kocha mpya ilikuhakikisha timu hiyo inafuzu kwa kombe la dunia litakaloaanza mwezi ujao mjini Rio Brazil .

Kocha Mpya

Mjerumani Thomas Rongen ndiye aliyekabiliwa jukumu la kufufua hadhi ya kandanda katika kisiwa hicho mbali na kukomesha msururu wa matokeo duni na kushindwa katika kila mechi waliocheza ya kimataifa .

Kocha huyo alianza kwa kuwasaili wachezaji wliokuwepo katika mechi hiyo ya kihistoria huku akifahamu kuwa matamanio ya takriban wasamoa eflu 65 yalikuwa mabegani mwake .

Image caption Kocha mjerumani Thomas Rongen aliyeifufua timu ya Samoa

Aidha moyo wa wachezaji na motisha waliokuwa nao ilimshangaza kocha Rongen. ''Itakuwaje mtu anawania kuiwakilisha taifa lake katika kikosi ambacho kimeshindwa katika mechi zote ?''

Kiungo Jaiyah Saelua aliyeshiriki katika mechi hiyo alisema hata ingawa hawakuwa na viwango vya ushindani kama wachezaji wapinzani wao ilikuwa jambo la kujivunia kuvalia jezi la taifa.

Kila mtu alimshauri kocha huyo anayeishi marekani dhidi ya kuchukua wadhfa huo kwani ingemletea fedheha.

Hata mkewe alimzomea kuwa punguani endapo atachukua hatamu American Samoa.

Image caption Timu ya taifa ya Samoa

Lakini Mjerumani huyo alitua Samoa kwa kishindo na kuanza kazi na wachezaji waliokuwepo huko akiwemo mwanamke Jaiyah Saelua, aliyezaliwa kama mwanaume akiitwa Johnny,lakini maumbile yake yakabadilika na kuwa ya kike.

Kwa ufupi mwaka mmoja tangu hapo Novemba 2011, American Samoa ilisajili ushindi wake wa kwanza katika historia yake kwa kuandikisha ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Tonga.

Ushindi huo ulikuwa wa kwanza baada ya kushindwa katika mechi 30 zilizochezwa katika kipindi cha miaka 20.

Kocha Thomas Rongen aliongoza timu hiyo kusherekea ni kama walioshinda kombe la dunia akisema kuwa hiyo kwa hakika ilikuwa ni historia .

Timu hiyo ilijizolea pointi 18 na ikaimarika hadi nafasi ya 197 kati ya mataifa 209 yanayoorodheshwa na shirikisho la soka duniani FIFA.

Nafasi ya mwisho 207 inashikiliwa kwa pamoja kati ya mataifa matatu Bhutan ,San Marino na visiwa vya Turks & Caicos .