Uuzaji wa Tiketi za Madola waahirishwa

Image caption Uuzaji wa tiketi za Madola wasimamishwa

Waandalizi wa mashindano ya jumuia ya madola mwaka 2014 huko Glasgow wamefunga mtandao wake wa kuuza tiketi ili kutanzua kwanza tatizo lililopo la uuzaji tiketi.

Glasgow 2014 inasema kuwa tahadhari hiyo ni bora ili kuangazia maswala tata yanayotatiza uuzaji wa tiketi zingine za ziada zipatazo elfu kumi tangu siku ya jumatatu juma hili.

Waandalizi wanasema kuwa "poleni sana".

Kufikia sasa jumla ya tiketi elfu hamsini na tano zimeuzwa huku tiketi za ziada zikiwa zimenunuliwa hasa katika vitengo vya upigaji mbizi, kuogelea, uendeshaji wa baiskeli milimani, Uendeshaji wa baiskeli kwenye uwanja na urukaji zikiwa zimemalizika.

Image caption Uuzaji wa Tiketi za Madola waahirishwa

Mkurugenzi mkuu wa mashindano hayo David Grevemberg ameiambia BBC kuwa mtandao na laini ya simu ya uuzaji tiketi zitasalia kuwa kimya tangu saa kumi na mbili Jumanne wiki hii hadi pale swala hilo litakapotatuliwa.

Uuuzaji wa tiketi mtandaoni kwa mara ya kwanza ulianza rasmi jumatatu wiki hii.

Umaarufu wake kupitia mitandao ya kijamii ulisababisha kununuliwa kwa kasi huku wauzaji wakashindwa na ununuzi huo mkubwa na wa haraka.

Watu wengi wanasema kuwa wamekuwa wakijaribu kununua tiketi kwa kipindi cha masaa 24 mtawalia.

Aidha kunao walio lalamikia matatizo ya simu katika uagizaji wa tiketi hizo.