Je, njia bora ya unyoaji ndevu ni ipi ?

Image caption Je, njia bora ya unyoaji ndevu ni ipi ?

Je wanaume wanyoe ndevu zao kuanzia juu ama chini ya kidevu?

Licha ya mitindo ya unyoaji wa ndevu , kujifunza kunyoa ndevu kwa usahihi bado ni changamoto kwa wanaume wengi wanaobaleghe.

Asili mia kubwa ya vijana waliobaleghe hawajaweza kunyoa ndevu zao kama inavyostahili, anasema Jolly Kelly .

Mkono wake uliokuwa umeshika kijembe ukitetemeka .

Uso ulikuwa umejaa pamba zenye madoa ya damu .

Baadhi ya vijana huchukua muda kuelewa mitindo ya mavazi .

Mwandishi jarida la Takes time Matthew Paris mwenye umri wa miaka 64 aliandika majuzi kuwa muuguzi mmoja wa magonjwa wa ngozi aliwahi kumueleza kuwa chunusi nyekundu zilizotanda usoni wake zilisababishwa na kunyoa

ndevu kuanzia upande usiostahili na akamshauri kuwa anapaswa kunyoa kuanzia upande wa juu wa mashavu karibu na nywele akielekeza kijembe kwenye kidevu chake kinyume na alivyokuwa akinyoa miaka 50 iliyopita.

Unaponyoa ndevu kutoka juu ukielekeza kijembe kwenye kidevu hufanya unyoaji kuwa rahisi, wa haraka na wenye matokeo mazuri , lakini unaweza kusababisha maumivu kuliko kunyoa ndevu kuanzia juu, anasema Matthew Gass

kutoka shirika la madaktari bingwa wa ngozi wa Uingereza .

Kadri wembe unavyoingia zaidi ndivyo mtumiaji anavyoweza kupata maumivu, kuota kwa ndevu ndani ya ngozi na hata kusababisha makovu, aliongezea.