Wanajeshi wamshambulia kamanda Nigeria

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wanjeshi hao wamemlaumu kamanda wao kwa kusababisha mauaji ya wenzao

Wanajeshi nchini Nigeria, wamemfyatulia risasi kamanda wao mkuu katika mji wa Maiduguri Kaskazini Mashariki mwa nchi.

Hata hivyo Meja Jenerali, Ahmed Mohammed alinusurika kifo. Shambulizi lilifanywa dhidi ya gari lake katika kambi ya jeshi ya Maimalari .

Wanajeshi hao walimlaumu kamanda kwa mauaji ya wanajeshi wenzao walioshambuliwa na kundi la Boko Haram na kuuawa.

Wakati huohuo, Rais wa Goodluck Jonathan amesema hayuko tayari kubadilishana wasichana miambili waliotekwa nyara na wapiganaji wa Boko Haram wanaozuiliwa katika magereza ya Nigeria.

Haki miliki ya picha REUTERS
Image caption Wazazi wa wasichana waliotekwa nyara na Boko Haram

Waziri wa serikali awali alikuwa amesema kuwa maafisa wa utawala walikuwa tayari kwa mazungumzo na Boko Haram lakini Rais Goodluck Jonathan amesisitiza kwamba swala hilo halitazungumziwa.

“Amesisitiza kwamba hataongea na Boko Haram kuhusu kubadilishana wasichana waliotekwa na wapiganaji wa kundi hilo wanaozuiliwa nchini humo,” alisema mwakilishi wa serikali ya Uingereza Mark Simmonds baada ya kukutana na Rais Jonathan kujadili namna ya kuwanusuru wasichana hao.

Hatua ya kutekwa nyara kwa wasichana hao katika jimbo la Borno tarehe 14 Aprili, imesababisha kero kubwa kwa jamii ya kimataifa kiasi cha kulazimisha baadhi ya nchi za kutoa wataalamu kusaidia serikali ya Nigeria kuwatafuta wasichana hao.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii