Sevilla ndio mabingwa wa Europa

Image caption Sevilla ndio mabingwa wa Europa

Sevilla ndio mabingwa wa ligi ya bara Uropa mwaka 2014.

Vigogo hao wa ligi kuu ya Uhispania la liga waliwalaza Benfica kutoka Ureno mabao 4-2 kwa mikwaju ya penalti.

Timu hizo zilikuwa zimetoshana nguvu suluhu bin suluhu katika muda wa kawaida na ziada katika mechi hiyo iliyochezewa mjini Turin Italia.

Ushindi huo ulidhibitishia mashabiki wa kandanda kote duniani ufanisi wa ligi kuu ya Uhispania La Liga kwani ulikuwa ushindi wa tatu kwa timu hiyo ya Sevilla katika kipindi cha miaka mitatu .

Kwa upande wake Benfica sasa itasubiri muda zaidi kwani hawajashinda katika fainali nane sasa.

Mara ya mwisho timu hiyo kushinda taji lolote barani Uropa ilikuwa ni miaka 50 iliyopita 1962 .

Mechi hiyo iliishia sare tasa na ulipowadia wakati wa kuamua kupitia mikwaju ya penalti ni kipa wa Sevilla Beto aliyeamua taji hilo litaenda Uhispania wala sio Ureno. Beto aliokoa mikwaju miwili ya Oscar Cardozo na Rodrigo na kuitunuku Sevilla taji la Europa kwa ushindi wa mabao 4-2.