Rais Goodluck Jonathan kuzuru Chibok

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wanahakati wamekuwa wakishinikiza serikali ya Nigeria kuhakikisha kuwa wasichana waliotekwa wanaachiliwa

Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan anatarajiwa kuzuru mji ulio Kaskazini mashariki mwa nchi wa Chibok ambako wasichana zaidi ya 200 wa shule walitekwa nyara mwezi uliopita.

Hii itakuwa ndiyo ziara ya kwanza inayofanywa na Rais Jonathan katika mji wa Chibok tangu wasichana hao watekwe nyara na kundi la kiislamu la Boko Haram.

Rais Jonatahan amekuwa akilaumiwa kufuatia kushindwa kwa serikali yake kuwakoa wasichana hao.

Hapo jana alipuuzilia mbali masharti ya Boko Haram ya kutaka kubadilishana wasichana hao na wanachama wa kundi hilo wanaozuiliwa na serikali.

Siku ya Alhamisi bunge la waakilishi nchini Nigeria liliongeza muda wa sheria ya hali ya hatari Kaskazini mashariki mwa nchi.

Mnamo siku ya Jumatatu, kundi la Boko Haram lilitoa kanda ya video iliyoonyesha wasichana zaidi ya miamoja huku baadhi ya familia za wasichana hao zikiwatambua watoto wao.

Siku ya Alhamisi familia za wasichana hao zilitoa wito wa wasichana wao kuachiliwa bila msharti yoyote.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii