Idadi ya waliouawa kenya yafikia 10

Image caption Watalii wa Uingereza waondoka nchini kenya baada ya taifa lao kutoa tahadhari y kuwa nchini humo.

Idadi ya watu waliopoteza maisha yao kufuatia milipuko miwili katika soko moja la mji mkuu wa kenya Nairobi imeongezeka.

Idara ya kukabiliana na maswala ya dharura nchini kenya imesema kuwa takriban watu 12 wameuawa huku zaidi 70 wakijeruhiwa kufikia sasa.

Mlipuko wa kwanza ulitokea katika gari moja la usafiri wa uma huku mwingine ukitokea ndani ya soko hilo la Gikomba.

Mlipuko hiyo ilifanyika karibu na eneo la Eastleigh ambalo raia wengi wa kabila la Somali wanaishi na kufanya kazi.

Ilitokea wakati ambapo mamia ya watalii wa Uingereza walikuwa wakiondoshwa nchini baada ya idara ya kigeni ya taifa hilo kuonya kwamba kenya inakabiliwa na tisho kubwa la mashambulizi ya kigaidi kutoka kwa waislamu wenye itikadi kali.

Tayari kampuni mbili za kitalii za Thompsom na First Choice zimefutilia mbali safari zote za ndege zinazoelekea katika mji wa pwani ya Mombasa.