24 wauawa nchini libya

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wanamgambo

Makabiliano makali nchini Libya yamesababisha vifo vya watu 24 baada ya jeshi la angani la taifa hilo kuanzisha mashambulizi ya angani na ardhini dhidi ya makundi mawili ya wanamgambo katika mji wa Benghazi.

Mashambulizi hayo yaliongozwa na kanali wa zamani Khalifa Iftar ambaye ameitaja oparesheni hiyo kama ya kuimarisha hadhi ya Libya.

Wafuasi wake wanasema kuwa baadhi ya vitengo vya jeshi la ardhini pia vilijiunga na oparesheni hiyo.

Lakini kaimu waziri mkuu Abdullah Al Thani aliishtumu oparesheni hiyo akisema haikuwa halali.

Ghasia hizo zimelazimu kufungwa kwa uwanja mkuu wa ndege wa mji huo.

Tayari taifa la Algeria limefunga ubalozi wake mjini Tripoli kwa hofu ya kushambuliwa kwa wajumbe wake.