Guinea Bissau yafanya Uchaguzi wa pili

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wagombea wafanya kampeni nchini Guinea Bussau kabla ya uchaguzi wa awamu ya pili.

Taifa la Magharibi mwa Afrika ,Guinea Bissau linafanya awamu ya pili ya uchaguzi wa urais hii leo.

Aliyekuwa waziri wa maswala ya kigeni Jose Mario Vaz alipata kura nyingi katika raundi ya kwanza ya uchaguzi huo lakini akashindwa kupata kiwango cha kura zinazohitaji ili kuibuka mshindi.

Hatahivyo anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Nuno Gomez Nabiam ambaye waandishi wanasema anaungwa mkono na jeshi.

Jeshi nchini humo lilifutilia mbali uchaguzi wa kidemokrasi mnamo mwaka 2012 na taifa hilo limekuwa na rekodi ya mapinduzi ya kijeshi.

Hakuna kiongozi aliyechaguliwa na raia ambaye amemaliza kipindi chake cha miaka mitano tangu taifa hilo lijipatie uhuru wake kutoka kwa Ureno miaka 40 iliopita.