Ushirikiano dhidi ya Boko Haram waanza

Haki miliki ya picha AP
Image caption Rais wa Ufaransa na viongozi wa mataifa ya Afrika Magharibi

Viongozi wa mataifa ya Afrika Magharibi wanaohudhuria mkutano wa dharura mjini Paris,wamekubaliana kuimarisha ushirikiano wao katika vita dhidi ya wanamgambo wa boko haram.

Mkutano huo uliomshirikisha rais wa Nigeria Goodluck Jonathan na wenzake wa Chad,Cameroon,Niger na Benin uliitishwa na rais wa Ufaransa Francoiz Hollande .

Rais Jonathan ameuambia mkutano wa wanahabari kwamba sserikali yake na ile ya Cameroon wataanzisha oparesheni za Ushirikiano katika mpaka wao.

Waandishi wanasema kuwa uhusiano mbaya kati ya majirani hao wawili,umewafanya wanamgambo wa Boko haram kukimbia na kujificha nchini Cameroon kila wanaposhambuliwa na majeshi ya Nigeria.