Putin aamauru majeshi kuondoka mpakani

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Vladimir Putin

Rais wa Urusi Vladimir Putin amewaamuru askari jeshi walioko karibu na mpaka wa Ukraine kuondoka katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ‘The Kremlin’, rais Vladimir Putin amesema kuwa vikosi vilivyoko katika sehemu za Rostov, Belgorod na Bryansk vinapaswa kurudi katika makao yao ya kudumu.

Urusi ilikuwa imetoa ripoti kama hiyo, lakini Nato ikasema kuwa hakuna mabadiliko yoyote yalifanywa.

Wanahabari wanasema kuwa kuondolewa kwa vikosi vya kirusi vya askari wasiopungua 40,000 katika mpaka wa Ukraine unaweza kueneza mgogoro ulioko nchini humo.

Haki miliki ya picha RIA Novosti
Image caption Putin kwenye kikao na maafisa wa jeshi

Kuwepo kwa vikosi vya kirusi kumesababisha hofu katika sehemu hiyo.

“Pamoja na kumalizika kwa mafunzo ya kijeshi yaliyopangwa majira ya machipuko... maeneo ya Rostov, Belgorod na Bryansk, Putin amemuamuru waziri wa usalama kuwaondoa polisi walioshiriki katika jaribio hilo,” ripoti ya Kremlin iliyopewa mashirika ya habari ya Urusi ilisema.

Hali ya hofu imezuka kati ya Urusi na eneo la Magharibi la Rose baada ya kuondolewa mamlakani kwa rais wa Ukraine aliyekuwa akiunga mkono Kremlin mwezi Februari, baada ya kuwepo kwa maandamono mijini.

Kujitenga kwa neo la Crimea kutoka kwa Ukraine kulizua vurugu.

Kwingineko, vita vimekuwepo kati ya serikali ya Ukraine na majeshi yanayounga mkono waliojiondoa nchini Urusi magharibi mwa Ukraine