Wamalawi wafanya uchaguzi mkuu leo

Wagombea wa uchaguzi  mkuu Malawi
Image caption Wagombea wa kiti cha urais nchini Malawi

Raia wa Malawi wanafanya uchaguzi mkuu hii leo katika uchaguzi ambao wagombea kumi na mmoja wanawania kiti cha urais dhidi ya rais Joyce Banda.

Bi Banda - ambaye aliingia madarakani miaka miwili iliyopita baada ya kifo cha rais Bingu wa Mutharika - alipendwa sana na umma wa Malawi awali , lakini sifa zake zilipungua kufuatia kashfa ya hivi karibuni maarufu kama Cashgate.

Bi Banda anakanusha kuhusika kwa namna yoyote ile na kashfa hiyo.

Wachambuzi wengi wa siasa nchini humo wanabashiri kuwa bado yeye ndiye anayependwa na wengi hususan ni umaarufu wake katika maeneo ya vijijini .

Uchaguzi huo unatarajiwa kuwa na mchuano mkali kuwahi kushuhudiwa katika taifa hilo la Malaw.