Wahisani kuijadili hali ya Sudan:K

Raia wa Sudan Kusini
Image caption Baadhi ya raia wa Sudan kusini

Wahisani wa kimataifa wanakutana nchini Norway leo kwa mkutano unaolenga kujaribu kuchangisha pesa za kusaidia kupunguza mzozo wa kibinadamu nchini Sudan Kusini.

Umoja wa mataifa unasema kuwa zaidi dola bilioni moja zinahitajika kuwasaidia watu milioni nne wanaokabiliwa na njaa.

Nchi zilizoandaa mkutano huo Marekani, Denmark na Uingereza zimekwisha ahidi kutoa takriban dola milioni mia tano.

Umoja wa Mataifa unasema watu wengi wamelazimika kula mizizi na nyasi na kwamba wanahitaji msaada wa dharura kabla ya kuanza kwa msimu wa mvua ambao hufanya maeneo mengi ya nchi kutopitika.

Vita vya wenyewe kwa wenyewe vimesababishwa na uhasama kati ya makabila mawili , huku kila upande ukichangia katika kufanya mzozo huo kuwa mbaya zaidi .

Kwa pamoja rais , Salva Kiir na hasimu wake makamu wa zamani wa rais , Riek Machar, wanasema wameazimia kuheshimu mapatano ya hivi karibuni ya usitishaji mapigano.