City wamuudhi Toure

Haki miliki ya picha Getty
Image caption City wamuudhi Toure

Wakala wa kiungo wa Machester City Yaya Toure amekashifu kupuuzwa kwa kiungo huyo kutoka Ivory Coast.

Dimitri Seluk alikashifu ujumbe wa kheri njema kwa Toure ambaye alikuwa anaadhimisha siku kuu ya kutimiza miaka 31 mnamo mei tarehe 13.

Ujumbe huo ulioambatana na keki haukumridhisha hata kidogo Seluk ambaye anasema kuwa alitarajia wamiliki wa klabu hicho angalau kumtambua kiungo huyo wa Ivory Coast ,timu hiyo ilipotua Abu Dhabi kusheherekea ushindi wao wa taji la Uingereza kwa mara ya pili katika kipindi cha miaka mitatu.

Image caption Yaya Toure ameudhika Man City

Seluk alisema Toure huenda akaondoka iwapo wamiliki wa klabu hiyo wataendelea kumpuuza.

Toure aliandikisha kandarasi mpya ya miaka minne mwaka uliopita licha ya Seluk ambaye amemuakilisha Toure kwa zaidi ya miaka kumi kutishia kuwa kiungo huyo wa Ivory Coast angehama Etihad.

Uhusiano baina ya mchezaji huyo bora barani Afrika na Seluk umedumu kwa miaka mingi kiasi ya kuwa Toure alimpa mwanawe wa pili jina la Seluk.