Huwezi kusikiliza tena

Shauku kubwa ya matokeo ya uchaguzi Malawi

Siku ya pili baada ya uchaguzi mkuu Malawi na kura zingali zinahesabiwa. Kumeshuhudiwa matatizo ya kiufundi huku bado kuna baadhi waliokosa kupiga kura hata baada ya tume kutangazwa kwamba wangepiga kura hiyo hapo jana. Matokeo yasio rasmi yanaashiria kuongoza kwa kiwango kidogo Peter Mutharika, ambaye ni kakake aliyekuwa rais wa Malawi Bingu wa Mutharika, aliyefariki 2012. Rais Joyce Banda amekabiliwa na ushindani katika uchaguzi uliogubikwa na kashfa ya rushwa ambayo serikali yake inatuhumiwa kwayo. Anakana kuhusika kwa namna yoyote katika kashfa hiyo.

Msikilize Baruan Muhuza akiwa Lilongwe