Walimu waandamana Nigeria kutetea wanafunzi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Maandamano yamefanyika kote duniani kutaka wasichana waliotekwa nyara kuachiliwa

Walimu nchini Nigeria wanafanya maandamano ya siku moja kushinikiza serikali kuharakisha juhudi zake za kuwatafuta wasichana waliotekwa nyara na kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Boko Haram zaidi ya mwezi mmoja uliopita.

Maandanamo hayo pia ni ya kupinga mashambulizi ya Boko Haram dhidi ya walimu.

Kiongozi mmoja wa walimu hao aliambia BBC kwamba zaidi ya walimu miamoja sabini wameuawa mwaka huu.

Alituhumu maafisa wa serikali kwa kutoongeza juhudi za kuwalinda walimu na badala yake kujihusisha zaidi na siasa.

Wakati huohuo, Marekani imetuma vikosi vyake nchini Chad , nchi ambayo inapakana na Nigeria kama sehemu za juhudi zake kusaidia katika kuwatafuta wasichana waliotekwa nyara.