Waasi wa Tuareg watwaa mji muhimu Mali

Wapiganaji wa Tuareg Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wapiganaji wa Tuareg wakipeperusha bendera ya chama chao cha MLNA

Waasi wa Tuareg nchini Mali wamepata ushindi dhidi ya vikosi vya serikali katika mapigano makali ya kuutwaa mji muhimu wa kaskazini mwa taifa hilo wa Kidal.

Wanajeshi kadhaa wa serikali wameuawa ama kutekwa nyara , alisema msemaji wa wa waasi .

Serikali imekiri kuwa vikosi vyake vimerejeshwa nyuma na kwamba rais ametoa wito mapigano yasitishwe mara moja

Mapigano hayo yalizuka mara ya kwanza Jumamosi wakati waziri mkuu wa Mali Moussa Mara alipotembelea mji wa Kidal kuonyesha uungaji mkono kwa vikosi vya serikali vilivyoko mjini humo .

Mapigano hayo mapya yanatishia kumaliza juhudi za mazungumzo ya amani na waasi , wa vugu vugu linalopigania ukombozi wa Azawad (MNLA) .

Kundi hilo linapigania kujitenga kwa eneo la kaskazini mwa Mali.