Costa arejea mazoezini Atletico

Image caption Je Kondo la Nyuma ni dawa

Je Kondo la Nyuma ni dawa ?

Nyota wa Atletico Madrid Diego Costa amerejea mazoezini leo kujifua tayari kwa fainali ya kombe la mabingwa bara Uropa dhidi ya Real Madrid baada ya kudaiwa kuwa alizuru Belgrade kupata utabibu kutoka kwa Muuguzi mmoja anayetumia kondo la nyuma kwa utabibu wake.

Costa aliumia mapema katika mechi ya kuamua mshindi wa ligi kuu ya Uhispania la liga ambayo Atleticoilitoka sare ya 1-1 na Barcelona na kutawazwa mabingwa..

Image caption Je Kondo la Nyuma ni dawa

Mshambulizi huyo wa Uhispania alitafuta huduma za daktari huyo ambaye hutumia kondo la nyuma la farasi katika hospitali maalum huko Belgrade.

Costa amejijengea wasifu kwa kufunga mabao msimu huu akiorodheshwa kufunga mabao 36

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Simeone;Atletico inatafuta historia Lisbon

Kocha Diego Simeone alipata jeki kiungo chake cha kati kutoka uturki Arda Turan kurejea uwanjani kwa mazoezi saa chache kabla ya mechi kubwa zaidi katika Historia ya timu hiyo ya Atletico. Turan, na Costa wapo katika orodha ya wachezaji watakao tua Lisbon baadaye leo usiku.

Kwa upande wao Real walipata jeki baada ya kurejea kwa mchezaji bora barani ulaya Cristiano Ronaldo na mshambulizi Gareth Bale .

Ushindi huo wa kombe la La Liga la kwanza tangu 1996, umeimarisha matumani ya Atletico kutwaa kombe lao la kwanza.