Kenya yaweka mikakati ya kuinua utalii

Haki miliki ya picha b
Image caption Utalii nchini Kenya

Sekta ya utalii nchini Kenya inatarajiwa kuinuka kufuatia maagizo mapya ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.

Hatua hii inalenga kuikwamua sekta ya utalii ambayo imeyumba kutokana na vitisho vya hivi karibuni vya ugaini nchini humo.

Bwana Kenyatta alitangaza mpango rahisi na wa kuvutia kwa watalii wa ndani na wa kimataifa, ambapo watalii watalipa gharama kidogo watakapovinjari maeneo ya utalii wakati wa mapumziko.

Kwa mujibu wa maagizo hayo mapya , watalii watalipa gharama kidogo kwa tiketi za ndege , ada za kuzulu mbuga za wanyama, na pia itakuwa rahisi kwao kutembelea maeneo mbali mbali ya nchi.

Waajiri wametolewa wito kutoa likizo za mwaka kwa waajiriwa wao na gharama za mapumziko nchini Kenya .

Idara za serikali pia zina haki ya kuwa na furaha , na wameruhusiwa kufanya mikutano katika hoteli nchini, jambo ambalo lilipigwa marufuku takriban miezi miwili iliyopita kama moja ya hatua za kubana matumizi.

Raia wa Kenya watashuhudia matangazo zaidi ya utalii kwenye Televisheni, kama sehemu ya kampeni ya kuinadi Kenya.

Jukumu limesalia sasa kwa watalii kuchagua usalama au gharama za chini za kujivinjari.