UN:Vatican inapuuza haki za watoto

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis

Kamati ya Umoja wa Mataifa dhidi mateso imelaumu vikali kanisa Catholiki kwa kutoshughulikia ipasavyo suala la unyanyasaji wa ngono ndani ya kanisa hilo.

Katika ripoti iliyochapishwa hivi karibuni na Umoja huo mjini Geneva , Kamati hiyo imeushutumu utawala wa Vatican kwa kuwahamisha watawa kutoka parokia moja hadi nyingine kuwaepusha kushtakiwa, na kupuuza haki za waathiriwa za kupokea fidia .

Utawala wa Vatican uliithinisha mkataba dhidi ya unyanyasaji , ukatili na matendo yaliyo kinyume na utu.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Vatican inapuuza haki za watoto

Uchunguzi uliofanywa na kamati ya Umoja wa Mataifa dhidi ya Vatcan ni sehemu ya uchunguzi wa mara kwa mara wa kamati hiyo dhidi ya nchi wanachama ili kuhakikisha mikataba inatekelezwa.

Kamati hiyo ya Umoja wa Mataifa ina hofu kuwa wakati utawala wa Vatcan umeelezea kutokubali kamwe kuwepo kwa unyanyasaji ndani ya kanisa, maneno hayaendani na vitendo .

Kamati hiyo imekasirishwa zaidi na kwamba Utawala wa Vatcan unasisitiza kuwa unahusika zaidi na wahudumu wanaofanyika kazi ndani ya Vatcan kwenyewe , kuliko makasisi wake wanaofanyika kazi kwingineko duniani.

Mwezi Januari mwaka huu utawala wa Vatican ulichunguzwa upya na kamati ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watoto, baada ya kupokea ukosoaji kama huo kwamba ulishindwa kuwalinda watoto waliokuwa chini ya uangalizi wake.