Obama awazuru wanajeshi Afghanistan

Rais Obama akiwasili Afghanistan Haki miliki ya picha Reuters

Rais Obama anazuru Afghanistan ziara ambayo haikutangazwa kabla.

Amekwenda kuwaona wanajeshi wa Marekani katika kambi yao kuu Afghanistan huko Bagram, kabla ya wanajeshi hao kuondoka nchini humo mwisho wa mwaka.

Safari hiyo inasadifiana na Siku ya Kumbukumbu, ambapo Wamarekani wanawakumbuka wanajeshi wao waliokufa vitani.

Waandishi wa habari wanasema Bwana Obama anazuru Afghanistan wakati hasira inazidi nchini Marekani kuhusu namna wanajeshi wa zamani wanavyotendewa.