Shinawatra aachiliwa huru na Jeshi

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Yingluck Shinawtra

Kuna taarifa kuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Thailand, Yingluck Shinawatra, ameachiliwa huru na viongozi wapya wa jeshi, siku mbili baada ya kuwekwa kizuizini.

Duru ndani ya baraza la kijeshi linaloongoza nchi, zimeliambia BBC, kwamba Bibi Shinawatra, ameambiwa asijishughulishe na siasa, na anahitaji kibali akitaka kutoka nje ya nchi.

Bi Shinawtra alikuwa mmoja kati ya wanasiasa, wasomi na wadadisi, kama mia-moja-na-50, ambao walifungwa baada ya jeshi kunyakua madaraka Alkhamisi.

Wengi bado wako kizuizini.

Maandamano madogo lakini ya hasira, yameendelea kwa siku ya tatu mjini Bangkok, na kuzusha mapigano na baadhi ya watu kukamatwa, lakini hapakuwa na mapambano makali na askari wa usalama.