Anachotaka kufanya Jessica kabla ya kupofuka

Image caption Jessica akiwa na mamake

Mtoto mwenye umri wa miaka sita, ameorodhesha vitu ambavyo angependa kuona kabla ya kupoteza uwezo wake wa kuona kutokana na ugonjwa usio na tiba.

Jessica Smith anataka kuogelea na wanyama wa baharini wajulikanao kama Pomboo au 'Dolphines',kutembelea mbuga ya kuhifadhi Tumbili, na kuwa 'Princess wa Disney' kwa siku moja kabla ya kupofuka.

Mtoto huyo anaugua ugonjwa wa macho ujulikanao kama 'Leber's Congential Amaurosis' ambao unasababisha mtu kupoteza uwezo wa kuona anapoendelea kukuwa.

Orodha ya vitu ambavyo angependa kuona imesababisha Jesicca kuchangisha zaidi ya pauni 2,500.

Mamake Jessica, Kinsay,mwenye umri wa miaka 31, alisema kuwa aligundua kuwa macho ya Jessica yalikuwa na maji maji alipokuwa na miezi mitatu pakee na hapo akalazimika kuanza kuvaa miwani kuanzia umri wa miezi saba.

Mwaka jana alianza kulalamika alipoanza kuumwa na kichwa na miguu yake kuanza kufura huku ngozi yake ikiwa kama iliyogwaruswa.

Baadaye uchunguzi wa daktari ulibaini kuwa alikuwa anaugua ugonjwa huo.

Kwa usaidizi wa familia yake, mtoto huyo kutoka eneo la Merseyside, Uingereza,anaanza kujiandaa kwa maisha yake akiwa kipofu.

Alianza kujifunza kusoma kutumia Braille mwezi Septemba na pia akaanza kutumia kijiti anapocheza na dada zake.

Mtoto huyo pia anataka kutembelea hifadhi ya wanyama, kupigwa picha na kutembelea kampuni inayotengeza vifaa vya kuchezea watoto ya Legoland.

Wazazi wake nao wameanzisha mtandao ambao utawezesha Jessica kufikia ndoto zake kabla ya kupofuka