Pochettino ni mkufunzi wa Tottenham

Image caption Pochettino amekubali kandarasi ya kuwa kocha wa Tottenham

Tottenham Hotspur wamemwajiri Mauricio Pochettino kama mkufunzi wao mpya kwa mkataba wa miaka 5.

Pochettino anachukua nafasi ya kocha aliyefutwa kazi Tim Sherwood.

Raiya huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 42 alijiuzulu kutoka Southampton baada ya mwaka mmoja unusu katika klabu hiyo, na atakuwa mkufunzi wa 10 katika klabu ya Tot tangu mwaka wa 2001.

Msaidizi wake Jesus Perez, kocha Miguel D’Agostino na kocha wa walindalango Toni Jimenez pia wametoka Southampton ili kujiunga naye katika klabu ya Spurs.

Pochettino aliuambia wavuti wa Spurs kuwa klabu hiyo ilikuwa na sifa na historia nzuri sana, na kuwa alifurahia kupewa nafasi ya kuwa mkufunzi.

Kocha huyo wa zamani wa Uhispania alichukua usukani katika klabu ya Southampton mnamo mwezi Januari mwaka wa 2013 alipochukua nafasi yake Nigel Adkins, na kuwaongoza kumaliza katika nafasi ya 8 mwaka uliopita, matokeo mazuri zaidi katika historia ya klabu hiyo katika ligi ya Premier.

Luke Shaw, Adam Lallana, Rickie Lambert na Jay Rodriguezwote walipata nafasi ya kushiriki katika mechi za kimataifa chini ya mkufunzi huyo baada ya klabu yao kutwaa ushindi dhidi ya Manchester City, Liverpool na Chelsea.