Uchina na Vietnam wazozania nini?

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Eneo tata nambari HD981 la uchimbaji mafuta ndio kiini cha mzozo baina ya Uchina na Vietnam

Maafisa nchini Vietnam wanasema meli ya Chinese imeligonga na kulizamisha kwa kusudi boti la kuvua samaki la Vietnam katika eneo lilnalozozaniwa la kusini mwa bahari ya China.

Maafisa hao wamesema wavuvi kumi waliokolewa kutoka eneo hilo na hakuna aliyejeruhiwa.

Wanasema tukio hilo limetokea hapo jana kiasi ya kilomita 30 kutoka eneo kubwa la uchimbaji mafuta la China ambalo nchi zote zinadai kulimiliki.

Uchimbaji huo wa mafuta wa China umezusha mvutano kati ya Vietnam na China, na kumekuwa na visa vya maboti kugongana katika wiki za hivi karibuni.