'Wakimbizi' wauawa kanisani CAR

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waasi wa Seleka

Takriban watu 30 wameshambuliwa na kuuawa kanisani katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Walioshuhudia tukio hiyo walisema kuwa wapiganaji wa Seleka walirusha gruneti kabla ya kuanza kuwafyatulia risasi watu waliokuwa katika kanisa ya Fatima mjini Bangui kwa ubaguzi.

Wengi wa wapiganaji wa Seleka ambao ni wa dini ya Kiislamu wamekuwa wakijihusisha na vita vikali na wapiganaji wa Kikristo wa kundi la Anti-Balaka tangu mwezi Machi, 2013.

Vita hivyo vimewafanya takriban asilimia 25 ya wakazi wa Jamhuri ya Afrika kati kuwa wakimbizi.

Shambulio hilo kanisani limetokea saa chache tu baada ya vita kuzuka katika eneo la PK5 ambalo ni jirani na mji wa Bangui.

'Wakimbizi kanisani'

Walioshuhudia pia walisema kuwa watu waliokuwa kanisani walikuwa wakimbizi waliokuwa wakitafuta hifadhi kutokana na vita hivyo.

Image caption Waumini wa kiisilamu wlifukuzwa kutoka Bangui wakitishiwa kuuawa

Kasisi freddy Mboula aliambia waandishi wa habari wa AP (Associated press) kuwa alikuwa ndani ya kanisa vilio vya risasi vilivyoanza kusikika nje.

Kasisi huyo pia alisema kuwa kulikuwa na mayowe na baada ya dakika 30 ya milio ya risasi, miili ilikuwa imetapakaa kila mahali.

Kadhalika Kasisi huyo alisema kuwa idadi ya vifo huenda ikaongezeka kwa sababu ni watu wengi walipata majeraha.

‘Vita hivyo vingekuwa vibaya zaidi kama wanamgambo wa kupambana na Balaka hawangekuja kutulinda’ padri huyo aliongeza.

Wanakijiji kaskazini mwa mji wa Bamburi walipigana na wanajeshi kutoka Ufaransa Alhamisi ya juma iliyopita.

Waandishi wa AP walisema kuwa wanamgambo wa Kikristo walianza kuweka vizuizi barabarani karibu na Mji wa Bangui saa chache baada ya shambulizi hizo.

Shambulio hili dhidi ya wakristo ndilo mbaya zaidi nchini humo tangu wanamgambo wa Seleka kuondolewa madarakani Januari, 2014.

Michel Djotodia, alilazimishwa kujiuzulu kama rais baada ya kushindwa kuukomeshama shambulizi dhidi ya Wakristo.

Tangu siku hiyo, vitendo vya kulipiza kisasi dhidi ya waumini wa dini ya Kiislamu ambao walikuwa karibu kuondolewa kabisa mjini Bangui kwa kile Umoja wa Matifa unasema ni vita ambavyo vimechukua mkono wa kikabila.