Ford yaagiza magari milioni1 kurejeshwa

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Magari zaidi ya milioni moja yanahitilafu ya usukani

Kampuni kubwa ya kutengeza magari nchini Marekani imeagiza magari milioni 1.4 yarejeshwe kutokana na hitilafu ya usukani.

Takriban magari milioni 1.1 yaliyoundwa kwa mtindo wa kispoti yaliyokuwa yameuzwa Marekani Kaskazini yametakiwa kurejeshwa kwani huenda yana hitilafu kwenye usukani.

Vilevile magari mengine 200,000 yenye muundo wa Taurus yaliyoundwa kati ya mwaka wa 2010 na 2014 huenda yakakumbwa na tatizo ya kushika kutu kwa haraka.

Matukio kama hayo yaliyofanyika majuzi huenda yakaifanya kampuni hiyo kuvunja rekodi ya kutaka magari mengi zaidi yarejeshwe katika kipindi cha mwaka mmoja.

Haki miliki ya picha FORD
Image caption Magari zaidi ya milioni moja yanahitilafu ya usukani

Urejesho huo umetokea wakati sakata ya usalama inawakumba wapinzani wakuu wa kampuni ya hiyo , General Motors (GM).

GM ililaumiwa kwa kutotoa ilani za kiusalama kwamba baadhi ya magari yake hata baada ya kubaini kuwa magari hayo yanazima ghafla.

Dosari hiyo imehusishwa na vifo 13, ingawa wasanifu wa Marekani wanaamini kuwa idadi hiyo itaongezeka.

Pindi tangazo hilo lilipofanywa, kampuni za kutengeneza magari hayo pamoja na wasanifu wa Marekani wameongeza juhudi za kurejesha magari ambayo yanapatikana kuwa na dosari.