Mume atumai mkewe atanusurika kifo Sudan

Image caption Mwanamke aliyehukumiwa kifo kwa kuasi Uislam Sudan

Mume wa mwanamke aliyehukumiwa kifo kwa kuuasi uislamu na kuolewa na mkristo, ameielezea BBC juu ya matumaini yake kwamba rufaa yake itafaulu.

Dani Wani, mumewe Meriam Yahya Ibrahim, amemtembelea mkewe jela anakozuiliwa ambako amejifungua mtoto wa kike.

Image caption Dani Wani na wanawe, ameelezea matumaini yake kuwa rufaa ya mkewe itafaulu.

Amesema anahudumiwa vyema lakini mazingira hayo ya jela yamemuathiri sana mtoto wao wa kwanza.

Hukumu hiyo ya kifo kwa mwanamke huyo imeshtumiwa vikali na jamii ya kimataifa.

Ni matumaini yao kuwa rufaa hiyo itafaulu kabla ya mda wa miaka miwili aliyopewa kumwezesha kumnyonyesha mwanawe ipasavyo kukamilika.

Meriam alishtakiwa kwa kukataa kuurudia uislamu.

Nchini Sudan mwanamke wa kiislamu haruhusiwi kuolewa na mume asiyekuwa muislamu.