Vita vya Syria vimeuwa maelfu Allepo

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Syria imeshtumiwa kwa kuvurumisha mabomu maeneo ya makaazi.

Kikundi cha wanaharakati wa Syria wamesema kuwa mabomu yaliyorushwa na majeshi ya serikali katika kijiji kinachoaminika kuwa ngome ya waasi mwanzoni mwa mwaka huu, yamewaua zaidi ya watu elfu mbili.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wengi wa watoto wa Syria wamefariki na wengine kuathirika sana huku juhudi za kumaliza vita hivyo zikigonga mwamba.

Kikundi hicho kilicho na makao yake nchini Uingereza kimesema kuwa takriban mia tano kati ya waliouawa katika kijiji hicho kaskazini mwa Aleppo ni watoto chini ya miaka kumi na nane.

Kikundi hicho cha kutetea haki za binadamu kimeelezea jinsi mabomu hayo hutiwa ndani mizigo ya taka za vyuma na kuongezewa vilipuzi kisha kuvurumishwa kutoka juu angani hivyo kusababisha uharibifu mkubwa katika sehemu zinazolengwa.

Umoja wa mataifa umekariri kuwa utumiaji wa mabomu makubwa katika ya maeneo ya makaazi ya raia umepigwa marufuku chini ya sheria ya kimataifa ya haki za binadamu.