BBC yabaini ongezeko la wahamiaji Afrika

Image caption Wakimbizi wafrika wanaingia bara Uropa

BBC imebaini kuwa Kumekuwa na ongezeko kubwa la idadi ya wahamiaji wanaofika ulaya katika miezi ya hivi karibuni.

Kwa mujibu wa shirika la mpaka la Muungano wa Ulaya Frontex, Idadi kubwa ya wakimbizi hao ni wale wanaojaribu kuvuka kutoka kaskazini mwa Afrika wakielekea Italia.

Idadi ya wahamiaji imeongezeka katika ''msimu wa uhamiaji'' ambao bado haujafikia kikomo.

Mwishoni mwa wiki ongezeko kubwa la wahamiaji lilishuhudiwa kwenye vituo vya uhamiaji vya Uhispania na Ufaransa.

Ongezeko la wakimbizi lilianza miezi michache iliyopita ya mwaka wa 2013 na limeongezeka bila kupunguka muda huo wote.

Kulingana na shirika la Frontex wahamiaji 42,000 waliingia ulaya, kinyume cha sheria miezi minne ya kwanza ya mwaka huu, wengi wao wakipitia njia hatari za kuvuka Bahari kutoka Libya hadi Italia.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wakimbizi kutoka Kaskazini mwa Afrika wakiingia Lampedussa

Tangu wakati ule idadi ya wahamiaji imezidi kuongezeka.

Mnamo Jumatano, Serikali ya Italia ilisema kuwa idadi ya wahamiaji imepanda na kufikia 39,000.

Hii inamaanisha kuwa idadi ya wahamiaji kupitia njia mbadala hivi sasa imezidi 60,000.

Naibu Mkurgenzi Mtendaji wa Frontex, Gill Arias Fernandez, amesema kuwa huku msimu za joto unapokaribia, kuna uwezekano mkubwa kuwa idadi hiyo itaongezeka zaidi.

Hata hivyo idadi kamili ya wanaotaka kuhamia Ulaya itategemea hali ya kisiasa na usalama nchini Libya, ambako repoti zinapednekeza kuwa kuna uwezekano wa kuwepo zaidi ya wahamiaji 300,000 waliosubiri kuvuka.