Uingereza yakemea hukumu ya kifo Sudan

Image caption Miriam Ibrahim na mumewe

Viongozi wa kisiasa nchini Uingereza akiwemo waziri mkuu nchini humo wamekemea hukumu ya kifo iliopewa mwanamke mmoja wa kikristo kwa kukataa kubadili dini yake.

Wameitaja hukumu hiyo kama ya kuudhi.

Mwanamke huyo Mariam Ibrahim anazuiliwa katika jela moja ambapo alijifungua mtoto wa kike juma hili.

Mwanawe wa kiume aliye na miezi 20 pia yuko naye katika jela hiyo.

Amekuhukumiwa kwa kuwacha dini yake baada ya kukataa kubadilika kuwa muislamu.

Bi Ibrahim ambaye ameolewa na mkristo pia amehukumiwa kuchapwa viboko 100 kwa kuzini kwa kuwa ndoa na mtu ambaye si muislamu si halali chini ya sheria za Sudan.