Beckham kurejea uwanjani

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Beckham kurejea uwanjani.

Aliyekuwa mchezaji wa Uingereza na Manchester United David Beckham amedokeza kuwa huenda akarejea uwanjani akiichezea timu yake inayoshiriki ligi kuu ya Marekani MLS Major League Soccer huko Miami.

Nahodha huyo wa zamani wa Uingereza 39 alistaafu mwezi Mei 2013 baada ya kucheza kwa miaka 20 iliyokamilikia Paris St-Germain.

Akizungumza na na kipindi cha BBC Beckham alisema hakujawahi kuwa na mchezaji mmiliki lakini haoni kwanini kusiwe naye.

Kipindi hicho kinamwangazia nyota huyo wa Uingereza akisafiri maili 800 kwa pikipiki ngalawa na kwa ndege kuelekea kwenye msitu mkubwa zaidi wa Amazon Marekani ya kusini katika ziara ya siku 12.

Beckham anasema kuwa amepumzika vya kutosha na kuwa anapania kurejea uwanjani siku moja ,akijiuliza baada ya kutizama mechi za mpira wa vikapu iwapo anaweza kurejelea hali ya ushindani hata baada ya kustaafu.

Aliwahi kuichezea Uingereza katika mechi 115.

Katika kandarasi yake alipokuwa akiichezea timu ya Los Angeles Galaxy Beckham alitia sahihi kipengee kinachomruhusu kununua timu moja katika ligi hiyo kwa pauni milioni £25m na sasa anaazimia kuzindua klabu huko Miami katika msimu wa 2016 ama 2017.