AFC Leopards na Victoria fainali

Image caption AFC Leopards na Victoria katika fainali huko Sudan

Wawakilishi wa Kenya katika kipute cha kuwania ubingwa wa kanda ya Afrika mashariki na kati miongoni mwa vilabu AFC Leopards inajiandaa kwa mechi ya kukata na shoka dhidi ya Sports Club Victoria University kutoka Uganda baadaye leo jioni mjini Khartoum Sudan.

Leopards ilijikatia tikiti ya fainali hizo baada ya kuibana Academie Tchite ya Burundi mabao 2-0.

Aidha Ingwe ilikuwa imeshinda mechi zake zote kabla ya kutimu hapo.

Ingwee iliilaza Mbeya City ya Tanzania (2-1) kabla ya kuiramba Defence FC ya Ethiopia (3-2).

Image caption AFC Leopards na Victoria katika fainali huko Sudan

Kinyume na Leopards iliyofungwa mabao 3 katika mechi za mchujo na hata ikacheza mechi ya nusu fainali ikiwa na wachezaji kumi uwanjani , Victoria Sports Club ilifuzu kwa fainali hiyo bila ya kufungwa hata bao moja .

Victoria iliadhibu Al Shandy ya Sudan bao 1-0 katika ile nusu fainali nyengine.

Kabla ya kuibana Police (Zanzibar) 3-0, ikaibana Malaika (South Sudan) 1-0 kabla ya kujikatia tikiti fa fainali kwa kuilaza Al-Shandy (Sudan)1-0.

Mshindi wamchuano huo wa mataifa yanayo ambata mto Nile atatuzwa dola $ 30 000 huku mshindi wa pili akipokea dola elfu $20 000 .