Wafuasi wa Altaf Hussain wakita kambi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wafuasi wa Altaf Hussain wakifanya maandamano

Maelfu ya wafuasi wa mwanasiasa mwenye ushawishi nchini Pakistan Altaf Hussain ambaye alikamatwa mjini London Uingereza siku ya Jumane wamekusanyika na kuketi kwenye mji wa Karachi kwa siku ya pili sasa.

Bwana Hussain anaongoza chama cha MQM kilicho na ufuasi mkubwa mjini Karachi.

Shughuli mjini Karachi zimekwama zikiwemo za usafiri wa umma huku maduka na bishara zikifungwa.

Mwandishi wa BBC anasema kuwa hofu imetanda mjini Karachi na maeneo mengine ya mkoa wa Sindh

Mwanasiasa huyo alikamatwa kufuatia madai kuwa alihusika na vitendo vya ulanguzi wa pesa na kwa sasa anafanyiwa matibabu kwenye hospitali moja mjini London . Hussain ameishi uhamishoni nchini Uingereza kwa zaidi ya miaka 20.