Platini akanusha alipokea hongo

Haki miliki ya picha AP
Image caption Makamu wa rais wa FIFA Michel Platini amepinga madai alihongwa

Rais wa shirikisho la soka barani Ulaya ambaye pia ni Makamu wa rais wa FIFA ,Michel Platini amekashifu Gazeti la Daily Telegraph kwa kuashiria kuwa alikutana na aliyekuwa Rais wa shirikisho la bara Asia Mohamed bin Hammam muda mchache kabla ya kura za kuamua mwenyeji wa kombe la dunia la mwaka wa 2022.

Bin Hammam ambaye kwa sasa amepigwa marufuku ya maisha kwa kushiriki ufisadi ,ana anashtumiwa kwa kuwahonga wanakamati iliwaipigia kura Qatar kuwa mwenyeji 2022.

Gazeti hilo liliripoti kuwa Platini alikutana na bin Hammam kisiri muda mfupi kabla ya kura za hizo mwaka wa 2010.

Makamu huyo wa Rais wa FIFA amemwandikia mhariri wa jarida hilo akifafanua kuwa ‘uvumi hauna misingi na unalenga kumharibia jina.

‘Ni jambo la kuogofya kuwa mazungumzo yangu na mwanachama wa kamati ya FIFA yamegeuzwa kuwa jambo la kitaifa,’ Platini alisema katika barua lililotolewa na UEFA.

Rais huyo wa UEFA alisema kuwa ‘bila shaka’ walikutana na Bin Hammam, mwenzake wa muda mrefu katika FIFA na kiongozi mwenzake katika shirikisho la soka mara nyingi mwaka wa 2010.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Makamu wa rais wa FIFA Michel Platini amepinga madai alihongwa

Alisema kuwa mada katika mazungumzo yake na Bin Hammam ilikuwa kuhusu uwezekano wake kugombea urais wa FIFA, na kwamba Bin Hammam alikuwa akijaribu kumshauri agombee wadhifa huo mwaka wa 2011.

Baada ya Qatar kuchaguliwa na bodi ya FIFA kuwa wenyeji wa Kombe la Dunia 2022, Bin Hammam alijaribu kumuondoa Sepp Blatter kama kiongozi wa bodi inayotawala maswala ya soka.

Bin Hammam alijiondoa siku kadhaa kabla ya kupiga kura mnamo mwezi Juni mwaka wa 2011 wakati FIFA ilipokuwa ikijiandaa kumuondoa kwa madai ya kuwahonga wapiga kura wa Caribbean ambapo Blatter alichaguliwa tena.

Bin Hammam alipigwa marufuku maisha kutoshiriki kwa njia yeyote ile shughuli za kandanda.