Pembe za ndovu zanaswa Mombasa

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Pembe 228 za ndovu zanaswa Mombasa

Serikali ya Kenya imenasa shehena kubwa zaidi ya pembe za ndovu 228 katika kisiwa cha Mombasa mwaka huu.

Shehena hiyo ya pembe za ndovu 114 ilipatikana katika bohari moja inayotumika na kampuni ya uchukuzi.

Mshukiwa mmoja alikamatwa katika tukio hilo.

Kupatikana kwa shehena hiyo kubwa ya meno ya ndovu inatilia pondo dhana inayotokana na utafiti wa mashirika yanayopigania kusitishwa uuzaji wa pembe za ndovu kuwa bandari za Mombasa Kenya Togo na Dar Salaam

Tanzania zinatumika kusafirisha pembe za ndovu kutoka kote barani Afrika kuelekea bara Asia.

Utashi wa pembe za ndovu na bidhaa zitokanazo na pembe nchini China na mataifa ya Mashariki ya mbali ndio unaochochea mauaji ya tembo katika mbuga na hifadhi mbalimbali barani Afrika.

Haki miliki ya picha REUTERS
Image caption Maafisa wadai pembe hizo zilikuwa njiani kuelekea Asia

Mbali na kuwa bidhaa ya thamani kubwa huko Asia na China pembe za ndovu hutumika kama dawa ya kienyeji .

Shehena hii ni kubwa zaidi kuwahi kukamatwa mwaka huu bandarini kulingana na afisa wa Huduma kwa wanyama pori nchi Kenya yaani (KWS) Paul Muya.

Afisa wa KWS alidokeza kuwa kuwa shehena hiyo kubwa ya ndovu ilitoka katika moja ya mataifa mbalimbali yanayotumia bandari ya Mombasa kusafirisha bidhaa zao kuelekea ughaibuni.

Mwezi Aprili,Serikali ya Kenya iliwasimamisha kazi kwa muda maafisa wakuu wa shirika la huduma kwa wanyama pori KWS kwa kile ilichotaja kuwa ni utepetevu kazini.

Serikali Kenya wakati huo ilisema kuwa itachukua mstari wa mbele kulinda wanyama pori.

Kulingana na takwimu nchini Kenya vifaru 18 na ndovu 50 wameuawa mwaka huu idadi sawa na ile iliyosajiliwa mwaka uliopita.

Wanaharaki wa kulinda wanyama pori wanadai kuwa idadi hiyo ni chini mno kwani visa vingi haviripotiwi.