Lupita kuigiza katika Americanah

Haki miliki ya picha a
Image caption Lupita kuigiza katika Americanah

Muigizaji nyota kutoka Kenya Lupita Nyong'oamejumuishwa katika wasanii watakaoigiza katika filamu ya Americanah inayotokana na kitabu cha mwandishi Chimamanda Ngozi Adichie.

Filamu hiyo kama ile ya ''12 Years a Slave'' iliyompelekea kichuna huyo kushinda tuzo la Oscars mwezi Februari itatengenezwa na kampuni ya Plan B inayomilikiwa na Muigizaji nyota na mtayarishi msimamizi wa filamu Brad Pitt .

Filamu hiyo mpya ya Americanah inaelezea mada ya mapenzi kati ya raiya wawili wa Nigeria ambao licha ya penzi kuchanuka kati yao wanatenganishwa na maswla ya uhamiaji .

Muigizaji huyo aliwaambia mashabiki wake kuwa ni heshma kubwa kwake kupewa nafasi ya kuigiza katika filamu hiyo inayotokana na kitabu cha bi Adichie.

Kitabu hicho cha Americanah, kiachoelezea maisha ya wapenzi wawili Ifemelu na Obinze, chenyewe kinasifa si haba.

Kitabu hicho kilishinda tuzo la ''US National Book Critics Circle Award mwaka uliyopita.

Image caption Lupita kuigiza katika Star Wars na Americanah

Aidha kimeteuliwa kuwa moja kati ya vitabu kumi bora na jopo la 'The New York Times Book Review.

Nyongo aliiambia BBC kuwa baada ya kukisoma kitabu hicho , alitamaushwa na jinsi Ifemelu na mpenzi wake Obinze,walivyostahimili majaribu mengi katika uhusiano wao .

Hali ambayo inawakumba waafrika wengi ambao kutokana na tamaa ya mafanikio wanakwenda ughaibuni kutafuta ajira na wengine kwa masomo ya juu.

Mbali na Americanah ,Adichie anajivunia tajriba ya uandishi wa vitabu vingine kama vile Purple Hibiscus na Half of a Yellow Sun,ambayo pia imefasiriwa na kuigwa katika filamu na muigizaji nyota katika 12 Years a Slave , Chiwetel Ejiofor.

Nyong'o aliwatamausha wapenzi wa filamu kote duniani aliposhirikiana na Ejiofor na kutwaa taji la Oscar katika 12 years a slave.

Nyongo vilevile amejiunga na wasanii katika filamu ya Star Wars