Emir wa Kano azikwa Nigeria

Image caption Marehemu Emir Al-Haji Ado Bayero

Mazishi ya Emir wa eneo la KANO kazkazini mwa Nigeria yamefanyika.

Al haji Ado Bayero mmoja wa viongozi wa kidini anayeheshimiwa sana nchini humo alifariki mapema siku ya ijumaa akiwa na umri wa miaka 83.

Ni kiongozi wa pili kwa ukubwa wa dini ya kiislamu baada ya Sultan wa Sokoto.

Mwili wake ulizikwa katika makaburi ambayo mababu zake walizikwa karibu na nyumba yake huko Kano.

Kiongozi huyo wa dini alikuwa mkosoaji mkubwa wa kundi la wanamgambo wa Boko Haram.

Al-Haji Ado Bayero, alikuwa mtawala wa Kano tangu mwaka 1963 na alifariki baada ya kuugua kwa mda mrefu.

Tangu wakati huo Nigeria imekabiliana na misukosuko ya mapinduzi ya kijeshi na ghasia zingine.

Alikuwa na umri wa miaka 83 na kutambuliwa kama kiongozi wa muda mrefu sana na mkongwe zaidi wa waisilamu katika jimbo hilo na pia alitambulika kama kiongozi wa pili mwenye ushaiwishi zaidi kwa waisilamu Nigeria

Haki miliki ya picha AFP Getty
Image caption Emir akiwa kwa Maombi katika jimbo la Kano

Marehemu Emir pia alitambuliwa kama kiongozi aliyependa amani.

Miaka miwili iliyopita alinusurika kwa tundu la sindano baada ya msafara wake kushambuliwa ambapo dereva wake na walinzi wake wawili walifariki.

Ilishukiwa kuwa kundi la wapiganaji wa kiisilamu wenye itikadi kali, Boko Haram, ndio waliomshambulia.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Emir akiwa na mwanamfalme wa Uingereza Prince Charles

Boko Haram wamewashutumu viongozi wa kijadi nchini Nigeria kwa kuwa vibaraka wa wanasiasa. Juma lililopita Emir wa Gwoza aliuliwa na kundi hilo ambalo limetekeleza mashambulizi mengi Kaskazini Mashariki mwa nnchi hiyo.

Mwandishi wa BBC Sa'ad Abdullahi mjini Abuja anasema kuwa emiralikuwa amerejea tu kutoka mjini London ambako alikuwa anapokea matibabu.

Maishani mwake alikuwa mfanyakazi wa banki, polisi, mbunge , balozi na mfanyabiashara maarufu.