Putin akutana na rais wa Ukraine

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Putin akutana na rais wa Ukraine Petro Poroshenko

Marais wa Urusi na Ukraine wameongea kwa mara ya kwanza.

Vladmir Putin na Rais aliyechaguliwa nchini Ukraine, Petro Poroshenko, walikutana kwa muda mfupi kabla ya chakula cha mchana katika maadhimisho ya miaka 70 tangu mataifa ya Ulaya kukombolewa kutoka kwa Wanazzi.

Maadhimisho hayo yanaendelea nchini Ufaransa.

Maafisa wa Serikali wa Ufaransa walisema kuwa katika mashauriano ya viongozi hao wawili ambayo hayakuwa rasmi yaliyoandaliwa na Rais Fransois Hallande, Bwana Putin na Bwana Poroshenko walikuwa wamekubali kuwa mashauriano juu ya kusitisha mapigano katika Ukraine Mashariki yatafanywa hivi karibuni.

Maafisa hao walieleza kuwa viongozi hao wawili walizungumza juu ya kuzorota kwa uchumi kunakotokana na ghasia za kisiasa nchini Ukraine.

Baadaye Kiongozi wa Ujerumani, Angela Merkel, amehimiza Urusi kutekeleza wajibu wake kupunguza uhasama unaoendelea kupanda nchini Ukraine.