Wimbo wa Stevie Wonder ni kitambulisho

Image caption BBC Kutumia nyimbo za Stevie Wonder kama kitambulisho

Wimbo wake Stevie Wonder, Another Star, utakuwa wimbo utakaopeana sauti mrejeo katika maonyesho ya BBC ya kombe la dunia.

Wimbo huo, pamoja na ule wa Kilatino , zitatumika kama nyimbo za kufungua vipindi vyote vya Kombe la Dunia Brazili 2014, vitakavyopeperushwa kupitia BBC.

Nndio mara ya kwanza kabisa kwa mwanamziki huyu, mwenye uri wa miaka 64, kukubali wimbo wake utumike katika namna hii.

Image caption BBC kupeperusha mechi za WC_2014 moja kwa moja

Wonder aliutoa wimbo huo kiasili, katika mwaka wa 1976, kwenye albamu yake iliyoshinda tuzo la Grammy mara nyingi, iitwayo Songs in the Key of Life.

Wimbo huo, kwa mara ya kwanza utachezwa kwenye kituo cha BBC One tarehe 11, Juni, saa ili kukitambulisha kipindi kinachoangazia kipute hicho cha kombe la dunia.

Mtayarishi mkuu wa kitengo cha michezo, BBC, Ian Finch alisema kuwa BBC ilikua yenye bahati kupewa ruhusa ya kutumia wimbo huo.

‘Wimbo huu unaonyesha kwa uzuri hisia za sherehe na furaha ambazo tutawaletea watazamaji wetu katika msimu huu wa kombe la dunia.’ Finch.

Haki miliki ya picha Erica Ramalho
Image caption BBC Kutumia nyimbo za Stevie Wonder kama kitambulisho

BBC itaonyesha kwa kina Kombe la Dunia.

Itaonyesha michuano ya moja kwa moja katika BBC One, BBC One HD na tovuti ya BBC Sport na BBCSwahili.

Michuano mingine itakua ikiendelea katika BBC Three, BBC Three HD na Red Button.

BBC Two na BBC Two HD zitaonyesha mchuano huo kwa kifupi masaa ya asubuhi, na pia marudio ya mchuano wote .