Aagiza maiti ikatwe miguu Afrika Kusini

Image caption Miguu ya maiti inasemekana ailikuwa ndefu sana na kukwaza waandalizi wa mazishi

Mwandalizi mmoja wa mazishi nchini Afrika Kusini,anayedaiwa kuwaagiza wafanyakazi wake kuikata miguu ya maiti moja aliyodai kuwa ndefu sana alifikishwa mahakamani Ijumaa.

Ronel Mostert anayemiliki chumba cha kuhifadhi maiti ambacho pia huendesha shughuli za mazishi, alitoa amri hiyo kwa lengo la kuhakikisha kuwa maiti hiyo ingetosha katika jeneza.

Anakabiliwa na kosa la kumkata miguu maiti.

Mfanyakazi mmoja aalimbia mahakama kuwa Ronel alimuagiza kuchukua kifaa kimoja cha kukata ili kuikata miguu hiyo ya marehemu na kwamba jambo hilo limekuwa likimsumbua sana kimawazo.

Mwili marehemu ulifukuliwa ili kusaidia katika uchunguzi wa polisi.