Waasi wapewa fursa ya kujisalimisha

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mojawapo ya kundi la waasi nchini DRC Congo

Serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imesema kuwa inataka kuwapa waasi wa kihutu kutoka Rwanda, fursa ya kusalimu silaha zao kwa amani katika harakati ya kulivunja kundi lao la FDLR.

Msemaji wa serikali Lambert Mende amesema kuwa fursa ya kusalimu silaha kwa hiari bado ipo.

Alikuwa akizungumza siku moja baada ya zaidi ya waasi 100 kujisalimisha mbele ya serikali katika mji wa kivu.

Msemaji wa waasi amesema kuwa kundi la pili litajisalimisha kwa serikali katika eneo la kivu siku ya jumatatu.

Mnamo mwezi Aprili Kundi la waasi wa FDLR lilitangaza kuwa linasitisha uasi wake dhidi ya serikali ya Rwanda.

Maafisa wa umoja wa mataifa wanasema kuwa kufikia sasa ni waasi wa vyeo vya chini pekee waliosalimisha silaha zao na wana wasiwasi kuhusu hatua hiyo.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii