Mwanamke ashambulia kambi Nigeria

Rais Goodluck Jonathan Haki miliki ya picha Getty

Mwanamke aliyejitolea mhanga alijiripua nje ya kambi ya jeshi, kaskazini-mashariki mwa Nigeria.

Wanajeshi wawili walijeruhiwa vibaya.

Afisa wa jeshi aliiambia BBC kwamba mwanamke huyo aliyevaa hijabu, alikaribia kambi kwa piki-piki katika jimbo la Gombe.

Aliripua bomu wakati akihojiwa na wanajeshi.

Mwandishi wa BBC katika eneo hilo, anasema siyo kawaida kwa mwanamke kushambulia kwa kujitolea mhanga nchini Nigeria, na jimbo la Gombe limekuwa salama kwa jumla.

Hakuna kundi lilodai kufanya shambulio hilo.

Lakini kundi la Waislamu la Boko Haram, limekuwa likilenga makambi ya jeshi na polisi.