Boko Haram labadili nia kuhusu wasichana

Haki miliki ya picha
Image caption Kiongozi wa kundi la Boko Haram nchini Nigeria

Kiongozi mmoja wa kanisa la kianglikana anayehusika katika majadiliano ya kuwaachilia huru mamia ya wasichana waliotekwa nyara nchini Nigeria amesema kuwa wengi wao wanazuiliwa nje ya taifa hilo katika kambi tatu tofauti.

Daktari Steven Davis ambaye ni raia wa Australia ameiambia BBC kwamba wenzake waliwaona baadhi ya wasichana hao ambao walikuwa wakioga na upande mwengine kuwapikia waliowateka kutoka kwa kundi la wanamgmbo wa Boko Haram.

Davis amesema kuwa majadiliano ya kutaka kuwachiliwa kwa wasichana hao karibia yafue dafu kabla ya baadhi ya makamanda wa kundi hilo kulipinga wazo hilo dakika za mwisho wakihofia kukamatwa.

Amesema juhudi zozote za kuwanusuru wasichana hao kwa nguvu hazitafua dafu.