Sony imeipiku Nintendo katika mauzo

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Sony imeipiku Nintendo katika mauzo .

Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka miaka nane, Sony imeipiku Nintendo, kwa msingi wa mauzo ya michezo.

Sony imeuza milioni 18.7 kwa mwaka wa kifedha ulioisha mwezi Machi ukilinganishwa na Nintendo iliyouza milioni 16.3 ya michezo ya video

Data hiyo iliripotiwa kwa mara ya kwanza na tovuti ya habari ya kibiashara ya , Japani

Msingi wa ripoti hiyo ni kutokana na takwimu iliyochapishwa na Nintendo mbele ya mkutano wa wanahisa, na pia taarifa ya mapato iliyotolewa hapo awali na Sony

Habari hizi sio za kushangaza.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Sony imeipiku Nintendo katika mauzo .

Mfumo wa mchezo wa nne (Play Station 4) wa Sony umeibuka na kuwa bora kwa michezo inayouzwa ijulikanayo kama wa siku za usoni ama za kisasa ‘new-gen’.

Lakini mahitaji ya mchezo ujulukanayo kama Wii U wa Nintendo uliyo na uwezo wa kisasa wa kugusa kioo umebakia nyuma ya mchezo ya Wii ya awali iliyokuwa kifaa maarufu zaidi kwa kizazi kilichopita.

Takwimu hizo pia zilikuwa pamoja na zile za mauzo za kitambo za 'Playstation 3' na Wii ya hapo awali pamoja na 3DS ya Nintendo na pia PS Vita za Sony

Image caption Sony imeipiku Nintendo katika mauzo .

Sony, Nintendo pamoja na mpinzani wao kutoka Marekani, Microsoft, watatangaza vyeo vipya wiki huu ili kuambatana na ile ya michezo ya video ya E3 jijini Los Angeles

Ripoti ya Nikkei ilifuatia tangazo kutoka Nintendo kuwa ilikuwa inafunga makao makuu ya Ulaya nchini Ujerumani.

Habari hizo zilifuatia ripoti za Nintendo ya kusajili hasara ya dola milioni 229 kwa mwaka wa kifedha ulioisha tarehe 31 mwezi Machi.