Taliban yakiri shambulizi Pakistan

Image caption Taliban yadai kutekeleza shambulizi katika uwanja wa Ndege wa Karachi

Msemaji wa kundi la Pakistan Taliban Shahidullah Shahid amenukuliwa akisema kuwa walitekeleza shambulizi hilo ilikumkumbusha rais wa Pakistan Nawaz Sharif kuwa bado wepo nchini humu na kuwa kundi hilo litaendelea kutafutia haki mamia ya watu wanaouawa bila ya hatia yeyote katika mashambulizi ya ndege zisizo na ruban kwa misingi ya kuwasaka wapiganaji wa wataliban.

Waziri katika jimbo la Sindh , Qaim Ali Shah alisema kuwa wapiganaji hao walikuwa wamejiandaa vilivyo kutokana na jinsi walivyotekeleza mashambulizi hayo katika eneo la wageni mashuhuri katika uwanja huo mkuu mjini karachi wa Jinna.

Inaaminika kuwa 14 kati ya wale waliuawa ni maafisa wa usalama huku duru zingine zikisema kuwa hata wahudumu wa ndege mbalimbali waliathiriwa katika mkasa huo.

Mali ya thamani kubwa iliharibika lakini hakuna ndege iliyoharibiwa katika mashambulizi hayo.

Kuna hofu kuwa bado kuna mshambuliaji mmoja au hata wawili ndani ya uwanja huo.

Haki miliki ya picha AFP GETTY
Image caption Taliban yadai kutekeleza shambulizi katika uwanja wa Ndege wa Karachi

Hata hivyo, Maafisa wanasisitiza kuwa sivyo.

Kwa sasa serikali imesema kuwa imedhibiti uwanja huo na kuwa sasa uko salama kwa usafiri wa ndege.

Ufyatulianaji risasi na makabiliano baina ya wapiganaji wa kundi la Pakistan Taliban na maafisa wa usalama wa Pakistan uliripotiwa kuanza upya muda mchache uliopita katika uwanja mkubwa kabisa wa ndege wa Pakistan ulioko Karachi.

Hii ni baada ya mashambulizi ya usiku kucha yaliyodaiwa kutekelezwa na kundi hilo la Taliban.

Takriban watu 19 waliuawa katika ufyatulianaji huo wa risasi, wengi wao wakiwa maafisa wa usalama wa uwanja wa ndege.

Maafisa wa usalama wa Pakistani wamesema kuwa washambulizi wote 10 waliuawa mwishowe na kuwa uvamizi huo ulikuwa umeisha.

Mwandishi wa BBC aliyeko Islamabad Shahzeb Jillani anasema uvamivi huo ulikuwa wa kijarisi na bila shaka wa kujitolea mhanga.

Huu ulikuwa uvamizi wa kijasiri katika uwanja mkubwa kabisa wa ndege nchini humo.

Baada ya zaidi ya saa tano za mapigano makali na ufyatulianaji risasi , mkuu wa usalama wa mji wa Karachi alisema kuwa wavamizi hao walikuwa wameshindwa.

Lakini kidogo baadaye, milio ya risasi na milipuko ilisikika tena na kuzua taharuki.

Waokoaji walionekana wakirudi tena katika eneo la mashambulizi hayo.

Vituo vya habari vilionyesha picha za moto na moshi ukifuka tena kutoka kwenye paa ya uwanja huo.