Teknolojia kuwasaidia marefarii Brazil

Image caption Teknolojia ya kipekee kuwasaidia marefarii Brazil 2014

Je unakumbuka bao la Frank Lampard mwaka 2010 kati ya Uingereza na Ujerumani lililokataliwa kuwa mpira haukupita laini ?

Una maana gani kusema mpira haikuvuka laini?

Najua unajiuliza ,lakini Kandanda ina matukio mengi ya ‘kama ingelifanyika hivi’ Ingelikuaje kama msimamizi wa laini angesema kuwa bao lake Geoff Hurst kwa Uingereza katika kombe la dunia mwaka wa 1966, halikua limeupita mstari wa lango?

Je Ujerumani ya Magharibi wakati huo ingelinyakua kombe la dunia la mwaka huo ama Uingereza ndiyo ingetawazwa mabingwa ?

Ingelikuaje ikiwa bao lake Frank Lampard dhidi ya Ujerumani katika kombe la dunia mwaka 2010 lingekubaliwa?

Je Uingereza ingelishinda mechi hiyo?

Matukio ya lango la goli kama haya yamewaacha mashabiki wengi wakiililia teknolojia kuwakomboa.

Hata ingawa suluhisho imetumiwa kwa miaka mingi katika michezo mingine,kama Tennis Cricketi na Raga hii itakua mara ya kwanza teknolojia ya lango la goli kutumika katika kombe la dunia .

Ni mfano mmoja tu wa jinsi kombe hili la dunia litakavyokua lenye teknolojia kubwa zaidi na lenye kujumuisha miundo mbinu ya teknolojia ya karne ya 21.

Kamera tele.

Image caption Teknolojia ya kipekee kuwasaidia marefarii Brazil 2014

Kampuni ya Ujerumani iitwayo GoalControl imeweka kamera 14 katika kila uwanja utakaotumika katika mechi za fainali za dimba hilo huko Brazil .

Kamera hizo zinauwezo wa kuchukua picha kwa kasi mno (saba kwenye kila lango), katika paa za nyanja zote 12, Brazili.

Kamera hizi zimeunganishwa kwenye tarakilishi inayounda maumbo na kuondoa umbo lolote lile ambalo sio la mpira, kisha kufuata mwenendo wa mpira kwa kadri milimita chache, kampuni hiyo ilisema.

Mpira unapovuka tu mstari wa lango, utakuwa unapeperusha ujumbe kwenye saa yake mwamuzi wa mechi, kisha ujumbe wenye maandishi ‘GOAL’ unatokea kwenye saa hiyo pamoja na mtikisiko (Vibration).

Haya yote yanafanyika kwa muda wa chini ya sekunde moja.

Mfumo huo ambao tayari ushajaribiwa na Fifa, katika kombe la Mashirika mwaka uliopita.

Kampuni ya Sony, ambayo inathamini mpango huo wa kiteknolojia wa Fifa, wameweka zaidi ya kamera 224, zenye uwezo mkubwa, ambazo zitaonyesha zaidi ya saa 2500 ya michezo.

Image caption Teknolojia ya kipekee kuwasaidia marefarii Brazil 2014

Hii itakua mara ya kwanza michuano ya kombe la dunia kuonyeshwa katika mfumo wa kisasa wa kiteknolojia wa Ultra-High Definition (UHD), ujulikanao kama 4K Format, ambayo kiwango chake ni mara nne zaidi ya kiwango cha

televisheni za kawaida.

Ilikufanikisha ubora huu wa picha waandalizi wameandaa muundo msingi wa mtandao wa interneti unaoweza kuhudumu kimo cha megabiti 100 kwa sekunde moja.

Hata mashabiki wengi hawatakua na uwezo wa kupokea mawimbi hayo ya 4K Format.

Hata hivyo , mkurugenzi mkuu wa vipindi vya kombe la dunia wa Sony, Mark Grinyer, aliliambia BBC kuwa wanapania kuweka daftari ya matukio yote huko Brazil katika mfumo huo mpya kwa nia ya kuboresha ubora wa picha kuambatana na teknolojia ya siku sijazo.

Mfumo huu unaubora mara nne zaidi ya ule unaonadiwa haswa barani Afrika kama Full HDTV .

Kombe lililounganishwa

Takriban mashabiki milioni tatu watashuhudia mechi hizo uwanjani huku Takriban Bilioni nne zaidi wakuutizama kwenye runinga .

Mashabiki zaidi watakua wakishiriki mazungumzo na mijadala na kuwekeana dau, kwa wakati mmoja, kupitia mitambo tofauti ya kidijitali.

Hili linalifanya kombe hili kuwa lile ambalo linaweza kutazamiwa kwenye aina nyingi ya mitambo na mifumo tofauti pia .

Makamu wa rais wa Akamai ambayo ni kampuni ya kutoa huduma ya mtandao, alisema kuwa jinsi watu wanavyoweza kutazama maonyesho imeongezeka.

Kuna vifaa vingi vilivyo na uwezo wa kutumia mtandao na watu wengi wanavitumia.

Mkuu wa teknolojia ya miundombinu katika kampuni ya Cisco Systems, Ian Foddering, alisema kuwa miaka miwili baada ya michezo ya olimpiki, matarajio ya watumizi wa mitambo hii ilikua imeongezeka kulingana na matukio kama haya.

Watazamaji sasa wana matarajio ya mitandao iliyo ya kasi na iliyoenea kote, ili kuwawezesha kutumiana matukio hayo kupitia mitandao ya kijamii.

Hili lina peana changamoto kwa wanaosambaza mitandao na kampuni za tarakilishi kwa pamoja.

Kivunja rekodi

Watengezaji wa chombo cha OneFootball, wameanzisha chombo kitakachotumika katika mashindano hayo.

Image caption Bao la Lampard lililokataliwa Afrika kusini 2010

Mkurugenzi mkuu Lucas von Cranach aliliambia BBC kuwa kombe hili la dunia litavunja rekodi kidijitali na kwa utumizi na binadamu.

Alizidi kusema kuwa wanatarajia chombo chao cha OneFootball Brasil kitakuwa na watumizi wengi.

Kampuni hiyo tayari imetengeneza mfumo wenye uwezo wa kuhudumia idadi kubwa ya watumizi.

Mfumo wao wa Amazon Web utawasaidia kufanikisha shughuli hiyo.

Mtumizi sharti ahakikishe tu kuwa kuwa wahudumu wa mitandao wanatoa huduma nzuri.

Akamai imesema kuwa inatarajia kuhudumia mitandao milioni 2.5 ya moja kwa moja katika kombe hili la dunia.

Hii ni ongezeko maradufu ikilinganishwa na milioni 1.6,waliohusika katika kombe la dunia mwaka 2010.

Kuweka nada kutaongezeka katika msimu huu wa kombe la dunia.

Skrill, ambayo ni kampuni ya kutoa malipo ya mtandaoni, imesema kuwa thuluthi ya watu wazima Uingereza wana mipango ya kuweka nada katika kombe hili la dunia.

Zaidi ya nusu ya idadi hii itafanya hivyo kupitia kwenye mitandao , na robo ya idadi hiyo, kupitia kwa vyombo vya simu za mkononi.

Thamani ya minada duniani kupitia simu za mikononi yatarajia kufikia dola milioni 62 itimiapo mwaka 2018.

Ongezeko mara sita zaidi ya ile ya mwaka wa 2013, kulingana na kampuni ya utafiti wa matumizi ya Juniper .

Kuweka minada kupitia kwenye vyombo vya mikononi kunatarajiwa kuleta pesa zaidi, kuliko njia nyingine zozote, kulingana na Tom Levy, wa kampuni ya AppDynamics.

Hili ndilo kombe la dunia la kwanza lililo la kidijitali kamili.

Uti wa mgongo wa Brazili

Image caption Teknolojia ya kipekee kuwasaidia marefarii Brazil 2014

Kampuni ya kimawasiliano ya Oi ambayo ni mshiriki wa Fifa katika kombe la dunia, imejianda kamili kwa kombe hili la dunia.

Mitandao yao imeongezwa na kufanywa kuwa kasi katika miezi michache iliyopita.

Msemaji wao aliliambia BBC kuwa wameongeza maeneo tete kutoka 78,000 mwezi Aprili hadi zaidi ya 700,000 sasa.

Hii ni idadi kubwa zaidi, ya mitandao katika nchi ya Brazili.

Kampuni hii pia imeongeza nguvu za mitandao yake ya 2G,3G na 4G katika

sehemu muhimu katika miji yote itakayoandaa michuano ya kombe la dunia.