Je azma ya Nkurunziza inakiuka katiba?

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Nkurunziza anasema kuwa katiba ya nchi hiyo inahitaji kufafanuliwa kuhusiana na yeye kuwania urais

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, amegusia kuwa huenda akawania urais kwa muhula wa tatu licha ya upinzani kulalamika kuwa hatua kama hiyo itakuwa inakiuka katiba.

Bwana Nkurunziza aliambia BBC kuwa maelezo katika katiba kuhusu jambo hilo hayaeleweki kwa misingi hiyo na kwamba yanahitaji ufafanuzi.

Alisema kuwa ikiwa chama chake kitamuomba kuwania urais kwa muhula wa tatu, litakuwa swala linalohitaji kufafanuliwa na mahakama ya kikatiba.

Hali ya wasiwasi ya kisiasa nchini Burundi katika miezi ya hivi karibuni kuhusu hatua ya serikali kujaribu kubadilisha katiba.

Wanachama wa upinzani, baadhi ambao wamekamatwa, wanasema hatua hiyo itawakera wengi hasa kwa msingi ya kikabila.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii