Majeshi ya DRC na Rwanda yakabiliana

Image caption Majeshi ya DRC yakabili wanajeshi wa Rwanda mashariki mwa Congo

Maafisa wakuu katika Jamuhuri ya kidemokrasi ya Congo wanasema kuwa makabiliano makali yalizuka mapema leo kati ya wanajeshi wa DRC na wanajeshi wa Rwanda.

Waziri wa mawasiliano, Lambert Mende, anasema kuwa makabiliano hayo yaliendelea kwa muda na kuendelea kwa saa kadhaa katika eneo la mpakani kati ya nchi hizo mbili.

Alisema makabiliano yalianza wakati wanajeshi wa Rwanda walipovuka na kuingia katika mkoa wa Kivu na kumkamata mwanajeshi wa Rwanda.

Hadi sasa hapajakuwa na tamko lolote kutoka kwa upande wa Rwanda.

Serikali ya Rwanda imetuhumiwa na Umoja wa Mataifa kwa kuhusika na mzozo unaotokota katika mashariki ya Jamhuri ya Congo.

Rwanda imekanusha adai hayo.